Friday, July 30, 2010

Best Blogger Tips
Mama Sitta: Takukuru wana lao

Via Mwananchi

SIKU moja baada ya Takukuru mkoani Tabora kutangaza kuwa imemnasa Margaret Simwanza Sitta kwa tuhuma za rushwa, waziri huyo wa Maendeleo ya Jamiii Jinsia na Watoto amejitokeza na kudai kuwa taasisi hiyo inawabambikia wananchi makosa ili ionekane wanafanya kazi.

Alisema kutokana na tukio lililompata juzi, sasa anawasiliana na wanasheria wake kuona achukue hatua gani dhidi ya maafisa wa Takukuru waliodai kumkamata kwa rushwa.

Waziri Sitta alisema kwamba juzi saa 7:30 usiku aliamshwa kwa mlio wa simu ya Catheri Sepetu iliyomwomba afike gesti ya Camise kuona mtoto mgonjwa.

"Niliomba anielekeze gesti hiyo iko wapi ili niende kumwona huyo mgonjwa," alisema Mama Sitta.

Mama Sitta alidai kwamba kutokana kutoyafahamu maeneo hayo alimwomba katibu mwenenzi CCM wa Tabora wafuatane katika maeneo hayo aliyoambiwa na Sepetu.

Alisema alipofika karibu na njia ya kwenda katika gesti hiyo, wakatokea vijana zaidi ya sita na kusimamisha gari alipowahoji nyie ni nani ndipo walipotoa vitambulisho na kujitambulisha kwamba wao ni Takukuru na kumweka chini ya ulinzi.

Alisema walimchukua hadi ofisini kwao na kuanza kumpekua huku wakimwambia alikuwa akigawa rushwa kwa wajumbe.

"Nikahoji huyo ndio mgonjwa mliokuwa mnaniitia? Hawakumjibu badala yake waliendelea kunipekua mkoba wangu na mkoba wa mdogo wangu na kumwamrisha katibu mwenezi, Rashid Ramadhan akubali kwamba alikuwa akigawa fedha," alisema Sitta.

"Katibu huyo alibaki anaduwaa kwani alichokuwa anajua ni kumsindikiza waziri kwa mgonjwa. Alishangaa kulazimishwa aandike maelezo kueleza kina nanni alikuwa anawagawia fedha. Akajibu siwezi kuandika wongo," alisema.
Endelea kusoma habari hii...................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits