Monday, July 26, 2010

Best Blogger Tips
Kocha mpya Stars aja Ijumaa

Via ippmedia

Kocha mpya wa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, Jan Poulsen, anatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa kwa ajili ya kuanza kibarua hicho kipya.

Poulsen ambaye ni raia wa Denmark, aliteuliwa kuwa kocha mpya baada ya Mbrazil, Marcio Maximo, kumaliza mkataba wake wa kuifundisha Stars uliodumu kwa miaka minne.

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, alisema kuwa mara baada ya kufika nchini, kocha huyo ataanza majukumu yake rasmi Agosti Mosi.

Tenga alisema kuwa anaamini kuwa wadau wa soka watampa ushirikiano kocha huyo mpya ili afikie malengo na Tanzania ifuzu kwa mashindano makubwa yajayo.

"Atakuja kati ya Ijumaa na Jumamosi, ila tulimweleza kwamba anatakiwa kuanza kazi Agosti Mosi, kikubwa ni kupewa ushirikiano kwa sababu yeye ni mgeni na mazingira ya hapa," alisema Tenga.

Kocha huyo ambaye alipita katika mchujo uliowashirikisha makocha 59 kutoka nchi mbalimbali, mtihani wake wa kwanza ni kampeni ya kuipeleka Tanzania katika fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika, ambapo Stars imepangwa kundi moja na nchi za Morocco, Afrika ya Kati na Algeria ambaye ilicheza fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika nchini Afrika Kusini.
Endelea kusoma habari hii......................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits