Wednesday, July 7, 2010

Best Blogger Tips
Salmin atua Dodoma na Siri moyoni

WAKATI hatima ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM inaelekea ukingoni mwishoni mwa wiki hii, makundi ya ushabiki yanahaha kuwapigia debe wagombea watatu ambao ni Dk Ali Mohamed Shein, Dk Ghalib Bilal na Shamsi Vuai Nahodha.

Jana rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Salmin Amour (Komando) aliwasili mjini Dodoma akiwa katika ndege moja na Waziri wa Kiongozi Vuai Nahodha ambaye ni mmoja wa wagombea.

Kwa muda mrefu sasa Dk Salmin haudhurii mikutana na vikao vya chama kutokana na kusumbuliwa na macho, hali inayoonyesha kuwa hatua ya sasa ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM ina unyeti wake.

Makundi hayo yameunda ushindani mkubwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM itakayofanyika kesho, mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka Dodoma wakati wajumbe na wagombea wanaendelea kuwasili, kuna mchuano mkali miongoni mwa makundi ya wapambe wao.

Fununu zaidi kutoka muongoni mwa wajumbe wa CCM zinasema kuna utofuati kati ya wajumbe wa Zanzibar na wa Bara kuhusu uungwaji mkono wa wagombea hao.

Uchunguzi umebaini kwamba, wafuasi wa vigogo hao wamekuwa wakitambiana na kuelekeza kampeni kwa wajumbe wa Halmashauri ya CCM (Nec), ambao ndio watakaopiga kura kumchagua mtu mmoja atakayeshindana na wapinzani katika kinyang'anyiro hicho.
Endelea kusoma habari hii...................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits