Thursday, July 1, 2010

Best Blogger Tips

Oprah Winfrey, atisha kwa utajiri

Mtangazaji wa televisheni Marekani Oprah Winfrey ametajwa kuwa mtu mwenye mvuto na utajiri mkubwa duniani kupitia jarida la Forbes. 

Winfrey amempiku muigizaji wa filamu Angelina Jolie kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya watu 100 mashuhuri kwa mwaka katika jarida la Forbes.

Nafasi hizo hupangwa kutokana na mapato ya mtu na kiwango anachoonekana kwenye vyombo vya habari.
Muimbaji Beyonce, amechukua nafasi ya pili, huku mkurugenzi wa filamu James Cameron akiingia tena kwenye chati na kuchukua nafasi ya tatu kufuatia mafanikio yake ya filamu ya Avatar

Lady Gaga amepanda katika nafasi mpya ya orodha hizo akiwa nafasi ya nne.
Kama ilivyo kwa Beyonce, mapato yake na taarifa za maisha yake kwa ufupi zimeongezeka katika miaka 12 iliyopita kutokana na ziara zake duniani na mikataba mbalimbali.

Jolie, wakati huo huo, ameteleza kutoka nafasi ya juu hadi kufikia nafasi ya 18.
Nyota wa gofu aliyezingirwa na matatizo mengi Tiger Woods ni nyota pekee wa michezo kuwa katika 10 bora.
Endelea kusoma habari hii.....................

 

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits