Saturday, February 26, 2011

Best Blogger Tips
Baraza la usalama kumuwekea vikwazo Gaddafi


Baraza la usalama la Umoja wa mataifa linakutana kuangalia uwezekano wa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi  serikali ya Kanali Muammar Gaddafi.

Baraza hilo linategema kuweka vikwazo vya kiuchumi na pia kutaifaisha mali za serikali hiyo.

Pia baraza hilo linapendekeza Kanali Gaddafi kufikishwa katika mahakama ya kimaifa ya makosa jinai  kwa makosa ya kukiuka  haki za binadamu.

Wakati huo huo, Rais Barack Obama wa Marekani, kwa mara ya kwanza amesema, Kiongozi huyo wa Libya anatakiwa kuachia madaraka na kuondoka katika nchi hiyo mara moja.

Ikulu ya Marekani imesema, Rais Obama aliweka msimamo wake wazi  wakati akizungumza na kiongozi wa Ujerumani  Kansela Angela Merkel wakati wa mazungumzo yao kwenye simu siku ya jumamosi jioni.

 “ Rais amesema, kama umefika wakati kiongozi unawaongoza watu wako kwa kutumia nguvu na unyanyasaji, ni kwamba umepotea maana halisi ya utawala na inatakiwa uitendee haki nchi yako kwa kuachia madaraka na kuondoka mara moja,” imesema taarifa hiyo.

Mapema, mmoja wa watoto wa Kanali Gadaffi, anayeitwa Saif al-Islam, alisisitiza kwamba  maisha yanaendelea kama kawaida  kwa robo tatu ya Libya. Taarifa yake inapingana na ya waandamanaji  wanaompinga Gaddafi ambao wanadai wameshikilia asilimia 80 ya nchi hiyo.

Ni vigumu kuthibitisha madai ya pande zote mbili, lakini inaaminika kwamba upande wa upinzani unashikilia mji wa pili wa Benghazi, wakati Kanali Gaddafi bado anashikilia mji mkuu Tripoli, ambao unakisiwa kuwa na watu milioni mbili. Nchi ya Libya inakisiwa kuwa na jumla ya watu milioni sita na laki tano.

Umoja wa Mataifa unakadiria zaidi ya watu 1,000 wamekufa katika uasi huo ambao umeingia siku ya kumi leo hii.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits