Thursday, February 10, 2011

Best Blogger Tips
Wabunge wa Chadema wamtikisa Pinda bungeni

WABUNGE wa Chadema jana walimtikisa waziri mkuu, Mizengo Pinda katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo wakimtaka kueleza serikali ina tamko gani kuhusu mauaji yaliyotokea Januari 5 mkoani Arusha.Kadhalika kikao cha tatu cha mkutano wa pili wa Bunge la kumi, jana kilishuhudia mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa mbunge wa kwanza katika bunge la kumi kuwekwa kikaangoni baada ya kupewa siku tano na Spika wa Bunge, Anne Makinda athibitishe madai yake kwamba Waziri Mkuu Pinda aliudanganya umma wa Watanzania wakati akijibu swali kuhusu vurugu za Arusha.

Hoja ya Mbowe
Msumari wa kwanza kwa Pinda, ulipigiliwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, baada ya kuuliza serikali inatoa tamko gani rasmi kuhusu tukio la mauaji ya watu watatu katika vurugu na maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na wahusika akiwamo IGP Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu.

Katika swali lake la nyongeza Mbowe alitaka kujua ni lini serikali itaunda tume ya kisheria kuchunguza tukio hilo kwa kupata maelezo kutoka pande zote husika tofauti na sasa ambapo taarifa zilizopo serikalini ni zile zinazotoka upande mmoja wa jeshi la polisi.

Majibu ya Pinda
Hata hivyo, akijibu kombora hilo, Pinda aliinyoshea kidole Chadema akisema kwa mujibu wa maelezo aliyopewa ilivunja makubaliano yake na polisi na kuandamana.

Pinda aliweka bayana kwamba, baada ya hali hiyo kilichotokea ni polisi kujaribu kuzuia maandamano hayo ya wanachama wa Chadema ambao tayari walikuwa wamehamasishwa na viongozi wao kwenda “kuwakomboa” wenzao waliokuwa wameshilikiwa kituo cha polisi mjini Arusha.

"Nakushukuru Mbowe kwa kuuliza swali hilo, serikali hii ni makini, ikiwa jambo limetokea usikimbilie kusema serikali,
serikali..., ni vizuri kuulizaa aliyesababisha...,'' alisema Pinda na kuongeza:

''Mlikiuka makubaliano na polisi, matamshi ya kwenye mkutano
hayakuwa ya chama chenye dhamira ya kujenga amani, mkawataka wafuasi waende kuwakomboa wenzao."

Katika kuondoa wingu na kuweka hadharani kila kitu, Pinda alisema pamoja na juhudi za polisi kuzuia maandamano hayo, lakini yaliendelea hadi mita 50 kutoka kituo cha polisi, nao hawakuwa njia nyingine kwa kuwa hawakujua nini kingewakuta kama waandamanaji wangevamia kituo cha polisi.
Endelea kusoma habari hii....................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits