Friday, February 11, 2011

Best Blogger Tips
Breaking News: Rais Mubarak wa Misri amejiuzuru


Maelfu ya watu wamelipuka kwa furaha baada ya Makamu wa rais wa Misri kutangaza kuwa Rais Hosni Mubarak ameachia ngazi.

Katika tangazo kupitia televisheni ya taifa, makamu wa rais Oma Suleiman amesema Bw Mubarak amekabidhi madaraka kwa jeshi.

Hatua hii imekuja baada ya maelfu ya watu kukusanyika mjini Cairo pamoja na miji mingine mikuu katika siku ya 18 ya maandamano ya kudai Bw Mubarak ajiuzulu.

Waandamanaji walipokea taarifa hizo kwa kushangilia, kupeperusha bendera, kukumbatiana na kupiga honi za magari. "Watu wameuangusha utawala," wamekuwa wakiimba.

"Kwa jina la Mungu mwenye neema, mwenye rehema, raia, katika wakati huu mgumu, Misri inapopitia, Rais Hosni Mubarak ameamua kuachia madaraka kutoka ofisi ya rais ya jamhuri na ametoa jukumu la kuendesha nchi kwa baraza kuu la jeshi," amesema.

"Mungu awasaidie wote,"

Bw Mubarak tayari ameondoka Cairo na yupo katika mji wa Sharm el-Sheikh, ambapo ana makazi mengine huko, maafisa wamesema.

Mjini Cairo, maelfu ya watu wamekusanyika nje ya Ikulu, katika eneo la wazi la Tahrir na katika kituo cha taifa cha televisheni.

Waandamanaji hao walikuwa na hasira kufuatia hotuba ya Bw Mubarak siku ya Alhamisi. Alikuwa akitarajiwa kutangaza kujizulu, lakini hakufanya hivyo na badala yake kupunguza madaraka yake kwa makamu wa rais.
 
Baada ya habari hizo kufika kwa wananchi, ambao wamekuwa wakiaandamana kushinikiza rais kujiuzuru mara moja, furaha kubwa iliibuka, ikiwa ni ushindi mkubwa kwao kwani matakwa yao yametimia.

Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel Mohammed El Baradei, ambaye alirejea Misri kujiunga na maandamano hayo, alisema, "Hii ni siku kubwa ya maisha yangu"

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits