Monday, February 14, 2011

Best Blogger Tips
Ronaldo atundika njumu

Mwanasoka mashuhuri wa Brazil, Ronaldo, ambae aliisaidia nchi yake kunyakua kombe la dunia 1994 na 2002, amethibitisha kuwa anajiuzulu kucheza soka.

Anaacha kandanda akiwa na rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika fainali za kombe la dunia kushinda mchezaji mwingine yeyote.

Ronaldo atakumbukwa kuwa ni mojawapo wa wachezaji hodari wa kandanda, ambaye aliwavutia mashabiki kila alikocheza kwa mbio zake karibu na lango na umahiri wa kufunga mabao.
Lakini sasa akiwa na umri wa miaka 34, Ronaldo anasema mwili wake haumruhusu tena kuendelea.

Katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya magoti ambapo mara tatu yalitishia kumzuia asiweze tena kucheza .

Katika kipindi cha miaka 18 iliyopita Ronaldo amefungia Brazil mabao 62 katika mechi za kimataifa,na kati hayo mabao 15 katika fainali za kombe la dunia, hii ikiwa ni rekodi.

Alionyesha ustadi wake kwa vilabu mashuhuri barani Ulaya, ikiwemo Barcelona, Real Madrid na Inter Milan.

Ametunukiwa tuzo ya FIFA ya kuwa mchezaji bora duniani mara tatu.

Alirejea Brazil akitumaini kukamilisha msimu wa mwisho katika michuano ya klabu.

Lakini maumivu yake na hali ya mwili wake ambayo ilimfanya asiweze kupunguza uzito wa mwili wake hatimaye vilimkatisha tamaa na akaamua asalimu amri.
Source: BBC

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits