Wednesday, February 2, 2011

Best Blogger Tips
Ghasia zachukua sura mpya Misri

Wafuasi wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak wamekabiliana na waandamanaji wanaomtaka kiongozi huyo aondoke madarakani katikati mwa mji wa Cairo.

Maelfu ya wafuasi wa Bw Mubarak walimiminika kwenye eneo la Tahrir na kuondoa vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na waandamanaji.

Pande hizo mbili zilirushiana maneno kabla ya kuanza kurushiana mawe.

Jeshi ambalo awali lilitoa wito kwa waandamanaji kutawanyika na kurejea katika shughuli zao za kawaida bado halijaingilia kati.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia walikuwa miongoni mwa baadhi ya wafuasi wa Bw Mubarak waliojitokeza katika eneo la Tahrir.

Mapambano mengine yameripotiwa kwenye mji wa Alexandria.
Source: BBC

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits