Sunday, May 1, 2011

Best Blogger Tips
Osama Bin Laden auwawa

Via BBC

Rais Barack Obama ametangaza kwamba wanajeshi wa Marekani wamemuua kiongozi wa mtandao wa Al Qaeda Osama BIn Laden. Obama amesema kundi la wanajeshi wachache wa Marekani walifanya operesheni iliyomlenga BinLaden katika eneo moja nchini Pakistan ambapo pia wamechukua maiti yake.

Wanajeshi wa Marekani wamekuwa wakimsaka Osama Bin Laden tangu kabla ya Mashambulizi ya Marekani ya Septemba 11, 2001 katika jengo la World Trade Centre na makao makuu ya kijeshi nchini humo, Petangon, na kuwaua zaidi ya watu 3,000.

Wasifu wa Osama Bin Laden

Osama bin Laden alizawa mwaka wa 1957, katika familia ya kitajiri nchini Saudi Arabia. Ana zaidi ya mandugu na dada 50. Babake Osama alimiliki kampuni kubwa ya ujenzi. Katika baadhi ya picha zake za utotoni, Osama ameonyeshwa akiwa na mavazi ya kifahari na ghali, akiwa likizoni katika miji mbali mbali barani Uropa.

Hata hivyo mwanzoni mwa miaka ya themaninialiyupia mgongo maisha haya ya starehe na kitajiri, ana kujiunga na vugu vugu la kupigania haki dhidi ya utawala wa kisovieti baada ya majeshi yake kuishambulia Afghanistan.

Na hapo akipigana pamoja na waarabu wenzake, ndipo alizindua kundi la kigaidi la Al qaeda. Mnamo mwaka wa 1998, alitangaza fatwa yaani vita vikali vya kidini dhidi ya Marekani. Kufuatia ghadhabu aliyokuwa nayo na Marekani, kwa kuweka majeshi yake katika ardhi ya kiislamu, katika nchi mbali mbali mashariki ya kati.

Alioa mke wake wa kwanza akiwa na miaka 17, na baadaye akawaoa ya wake wengine wanne. Osama Bin Laden naaminiwa kuwa na watoto 17.No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits