Monday, June 11, 2012

Askofu Malasusa: Wanasiasa msiteka nyara mchakato wa katiba

Best Blogger Tips
WANASIASA nchini, wametakiwa kuacha kujihusishana  suala la katiba na badala yake, suala hilo liachwe mikononi mwa wananchi.

Rai hiyo ilitolewa jana na jijini Dar es Salaam na  Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ,Askofu  Dk Alex Malasusa, alipokuwa akizungumz katia uzinduzi wa Usharika wa Kinyerezi.

Dk Malasusa alisema katiba  ya nchi si mali ya wanasiasa wanaotaka kuiteka nyara na kwamba hiyo ni mali ya Watanzania, wanaopaswa kupewa uhuru wa kujadili kwa kina.
Dk Malasusa alisema wananchi wanapaswa kuwa na fursa kubwa ya kuboresha mchakato  wa kuandika katiba hiyo, lakini wanakwamishwa na asilimia kubwa ya wanasiasa, wanachangia.

“Sina ugomvi na wanasiasa katika suala hili, ila  naomba wawaachie wananchi, kwanza ili wapate  fursa ya kuchangia maoni yao,”  alisema Dk Malasusa.Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuchangia maoni yao ili kuboresha  katiba inayotarajiwa kuandikwa kwa manufaa ya wananchi wote.

“Wote mjitokeze na kutoa maoni yenu, msikae kimya katika mchakato huu, alisema  Dk Malasusa.Pia aliwataka waumini wa kanisa hilo,  kubadilika na kufanya mambo yasiyomchukiza Mungu.Alisema lengi la kanisa hilo  ni kujaribu kuwasaidia waumini wake, ili  waweze kubadilika na si vinginevyo.
Chanzo: mwananchi

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits