Monday, June 4, 2012

Wahamiaji weusi washambuliwa Israel

Best Blogger Tips
 Wahamiaji wanne wa kiafrika wamejeruhiwa baada ya makaazi yao kuteketezwa na watu wanaoaminika kuwa wenyeji mjini Jerusalem, Israel.

Baada ya shambulio hilo ukawekwa ujumbe ukutani kuwataka wageni kuondoka eneo hilo. Katika siku za karibuni kumekua na hisia kali nchini Israel kuhusu jinsi ya kushughulikia wahamiaji elfu 60 kutoka Afrika.

Hapo Jumapili sheria mpya ilipitishwa kuwapa mamlaka maafisa wa uhamiaji kuwazuilia korokoroni wahamiaji haramu kwa miaka mitatu.Waathiriwa wa shambulio la sasa ni raia wa Eriterea ambapo walipata majeraha ya moto mikononi.

Msemaji wa polisi nchini Israel Micky Rosenfeld ameambia BBC kwamba kumekuwa na matukio mengi ambapo waafrika weusi wamekuwa wakilengwa na wenyeji.

Katika majuma ya karibuni ghasia zilitokea miji kadhaa ya Israel wanakopatikana wahamiaji wa kiafrika. Kusini mwa jiji kuu Tel Aviv biashara za waafrika zilishambuliwa huku waafrika wenyewe wakikejeliwa hadharani.

Polisi wanasema takriban wahamiaji elfu 60 wa kiafrika wanaishi Israel ambapo 35,000 wakikaa Tel Aviv na 5,000 wakiwa mjini Jerusalem.
Chanzo: BBC

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits