Wednesday, March 31, 2010

Best Blogger Tips
SAKATA LA KUHAMIA CCJ: Mtoto wa JK ajitosa kwa Mpendazoe

HATUA ya mbunge wa Kishapu Fred Mpendazoe kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama Cha Jamii (CCJ) imekipa kiwewe chama hicho tawala baada ya makada wake kutoa kauli zinazoashiria kumkebehi huku Ridhiwan Kikwete akiwatoa hofu wanachama wa chama chake.

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mohammed Mbonde, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa mikoa wa CCM, Pancras Ndejembi, mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan na wapigakura wa Jimbo la Kishapu jana walitoa kauli zinazotofautiana kuhusu uamuzi huo wa kihistoria.

Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, Ridhiwan Kikwete alisema kujiondoa kwa Mpendazoe kumeonyesha kuwa wananchi walikuwa na mbunge wa aina yake na kuwasihi wamwache aende zake.

Ridhiwan ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili mkoani Shinyanga kuhudhuria sherehe za kusimikwa kwa makamanda wa UVCCM wa wilaya, ziara ambayo imefanyika siku moja baada ya mbunge huyo kutangaza kuihama CCM na kujiunga na CCJ.

Alisema kuondoka kwa mbunge huyo kutoka CCM na kukimbilia CCJ ni kielelezo cha aina ya viongozi ambao wamekuwa mzigo kwa chama ambao wamekuwa wakipendekezwa na kuteuliwa kuongoza.

"Mwacheni aende Mpendazoe, kuondoka kwake kusitufanye kukosa raha sisi CCM, wapo wengi waliondoka na chama bado kipo imara, muhimu kusonga mbele,” alieleza.

Alisema Mpendazoe alikuwa akifanya mambo mengi kinyume na kanuni za chama na kuwaomba wananchi kutulia na kuangalia viongozi wengine, lakini akisisitiza kuwa walio makini na siyo wale wa kuja.

Ridhiwan alisema kuondoka kwa Mpendazoe kunapaswa kuwa fundisho kwao kuchagua viongozi wenye sifa za uongozi na wenye uwezo wa kuongoza na kutamba kuwa chama kinao wanachama wengi, hivyo wanaoondoka kwa sababu zao wajue kuwa CCM itaendelea kubaki pale pale bila ya kutetereka.
Endelea kusoma habari hii..........

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits