Thursday, November 4, 2010

Best Blogger Tips
Bungeni hapatoshi

BUNGE la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa linaweza kuwa na sura tofauti kiutendaji kwa kuzingatia matokeo ya kura za ubunge na urais zilivyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ikionekana kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekwishamudu vigezo vya kuongoza Kambi ya Upinzani Bungeni, kama kilivyo Chama cha Mapinduzi (CCM), Raia Mwema limebaini.

Kwa kadiri ya mwenendo wa matokeo, chama chenye kupata wabunge wengi ndicho kitakachoweza kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kile kitakachofuata kwa idadi ya wabunge kitaongoza Kambi ya Upinzani Bungeni. Mchuano huo wa ama kuongoza kambi ya upinzani au kuunda serikali sasa ni dhahiri ni kati ya CCM na CHADEMA.

Kwa mujibu wa mwenendo ya matokeo ya kura za ubunge, CHADEMA inaelekea kupata wabunge wengi zaidi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambacho awali ndicho kilichokuwa kikiongoza Kambi ya Upinzani Bungeni chini ya kiongozi wake, Hamad Rashid Mohammed.

Hata hivyo, katika Bunge la tisa lililovunjwa kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, CUF ilikuwa na uwezo wa kuunda Kambi ya Upinzani bila kushirikisha chama kingine cha upinzani na ilifanya hivyo mwanzoni mwa Bunge lakini baadaye chama hicho kiliwashirikisha wabunge wa vyama vingine ambayo ni CHADEMA, UDP na TLP.

Katika mazungumzo yake na Raia Mwema kuhusu mazingira hayo, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni aliyemaliza muda wake, Hamad Rashid Mohammed ameliambia Raia Mwema kwamba taratibu za sasa zinabainisha chama chochote cha siasa kinaweza kuunda kambi yake kama kitafikisha asilimia 12 ya wabunge wote wa Bunge.
Endelea kusoma habari hii................
Source: Raia Mwema

 

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits