Thursday, November 18, 2010

Best Blogger Tips
Chadema wasusia hotuba ya Rais JK Bungeni

Wabunge wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo wamesusia hotuba ya Rais Kikwete wakati alipokaribishwa na Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano kulifungua Bunge hilo.

Hata hivyo, wakati wabunge hao wa CHADEMA wakiongozwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, wenzao wa vyama vingine waliwazomea, huku wakishangilia kwa kupiga meza na kuimba CCM, CCM, CCM.

 Pia, wabunge wengine wa CCM pamoja na wale wa CUF, walihamia kwenye viti vilivyokuwa vimekaliwa na wabunge hao wa CHADEMA.

 CHADEMA wametangaza kutotambua matokeo yaliyompa ushindi Rais Kikwete na mpango wao wa kutoka nje wa Bunge, ulibainika mapema juzi.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits