Tuesday, November 16, 2010

Best Blogger Tips
Prince William Kufunga ndoa mwakani

 
MJUKUU wa Malkia Elizabeth II, Prince William ametangaza kufunga ndoa na mpenzi wake wa miaka mingi Kate Middleton.
 
Habari zilisema Prince William na Kate ambao wote wana umri wa miaka 28, walichumbiana rasmi mwezi uliopita nchini Kenya na wanatarajia kufunga ndoa yao mwakani.
 
 Kwa mujibu wa taarifa Prince William na Kate walikuwa wapenzi kwa kipindi cha miaka minane, ambapo baadhi ya watu walimpa jina la utani Kate, kwamba ni mwanamke aliyekuwa akisubiri bahati yake.
 
 Habari zinasema harusi hiyo inatarajiwa kuwa ya kubwa na kuizidi ya wazazi wa William iliyofungwa miaka ya 1980, kati ya Prince Charles na Princes Diana (ambaye ni marehemu).
 
 Prince William alimvika pete ya uchumba Kate Oktoba mwaka jana walipokuwa mapumzikoni nchini Kenya.
 
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband, wamepongeza hatua hiyo ya Prince William na Kate. William ni rubani wa ndege za jeshi.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits