Wednesday, November 3, 2010

Best Blogger Tips

Republican yashika udhibiti wa bunge


 Imekuwa siku muhimu kwa chama cha Republican nchini Marekani baada ya matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula kuangazwa. Baadhi ya maeneo muhimu ambayo yalikuwa ngome ya chama cha Democratic sasa yako chini ya chama cha Republican.

Chama hicho kimetwaa viti sita vya bunge la Senate kutoka kwa chama cha Democratic na katika bunge la wawakilishi wamepitisha idadi ya wabunge 118 wanaohitajika ili kuwa na idadi kubwa.

Hii ina maana kwamba spika mpya atakuwa John Boehner kutoka jimbo la Ohio.

Amesema kwa kuwa sasa chama chake kina idadi kubwa ya wabunge watajiandaa kufanya mambo kwa njia tofauti. Ameongeza kuwa watazingatia kupunguza matumizi badala ya kuongeza.

Hamasa kubwa inayoonekana katika kampeni za chama cha Republican imetoka kwa vuguvugu la Tea party ambalo limeundwa na wanaharakati.

Chama cha Rais Barack Obama kimepata pigo kubwa kama ilivyotarajiwa lakini pia wamejipatia ushindi katika maeneo machache ikiwa ni pamoja na Nevada ambapo kiongozi wa Senate Harry Reid alimshinda mpinzani wa vuguvugu la Tea party.

Baada ya kutangazwa mshindi seneta Reid alikiri kuwa kilikuwa kibarua kigumu kuhimili upinzani huo.
Rais Obama sasa atakabiliwa na changamoto kubwa katika kutimiza ajenda yake.
Source: BBC

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits