Sunday, November 7, 2010

Best Blogger Tips
Mziray: Aliondoka Tanga na African Sports yetu......


Via Raia Mwema

NYINGI  ya tanzia nilizosoma kuhusu upande wa michezo wa maisha ya marehemu Syllersaid Mziray aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita zimejikita zaidi kwenye mafanikio yake katika kuzifundisha timu mbili kubwa za soka nchini za Yanga na Simba za Dar es Salaam kwa vipindi tofauti.

Yameorodheshwa pia mafanikio yake kwenye timu ya taifa ambapo yeye alikuwa miongoni mwa walimu watatu ambao mwaka 1994 waliiwezesha timu ya taifa ya soka, Taifa Stars kutwaa Kombe la Challenge mjini na Nairobi baada ya kuwa tumelikosa kwa miaka 20 kabla ya hapo. Walimu wengine walikuwa ni Sunday Kayuni na Charles Boniface Mkwasa.

Syllersaid Mziray alikuwa ni miongoni mwa walimu wa soka wachache sana nchini ambao waliweza kuzifundisha timu mbili kubwa nchini za Yanga na Simba kwa nyakati tofauti na akaweza kufanya kazi yake kwa mafanikio makubwa bila fitna za timu hizo kumuathiri kwenye utendaji wake wa kazi.

Kwa hakika, kocha Mziray alikuwa kama kocha kiraka kwa timu hizo kutokana na ukweli kwamba mara nyingi timu zilipokuwa na matatizo ya kocha zilimkimbilia Syllersaid Mziray aokoe jahazi ingawaje pia mara kadhaa ilitokea kuwa hawakuachana vizuri.

Hata hivyo, maelezo mengi yanayohusu mchango wa kocha Mziray kwenye michezo yamesahau kurodhesha mchango wake muhimu sana katika soka ambao kwangu mimi ndio uliotengeneza jina lake na kuwa miongoni mwa makocha bora kabisa wazalendo tuliopata kuwa nao.

Kumbukumbu zangu kuhusu Mziray zinanirudisha miaka 22 nyuma, mwaka 1988, wakati alipokuja mjini Tanga kufundisha timu ya African Sports ya Tanga ambayo mwaka huo ilikuwa imepanda daraja na kuingia iliyokuwa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Katika kupanda daraja huko African Sports ilikuwa imemfuata mpinzani wake wa jadi mkoani Tanga Coastal Union ambaye tayari ilikuwa ‘mzoefu’ wa kucheza Ligi ya Daraja la Kwanza iliyokuwa ya juu kabisa kwa wakati huo.

Kupanda daraja kwa African Sports na kuwapo uhakika wa kukutana na mpinzani wa jadi nchini, Coastal Union katika msimu wa ligi ya mwaka 1988 kulileta msisimko wa aina yake mjini Tanga kwani kabla ya hapo timu hizo zilikuwa hazijakutana kwenye michuano mikubwa ya soka nchini.

Chini ya Mziray, African Sports ilisuka kikosi mahiri cha wachezaji kama Francis Mandoza, Bakari Tutu, Hassan Banda, Hamza Maneno, Mhando Mdeve, Raphael John, Juma Burhani, Victor Mkanwa, na kuweka kambi kwenye mji wa Korogwe wakifadhiliwa na kampuni ya Sikh Garage.
Endelea kusoma habari hii.................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits