Friday, November 12, 2010

Best Blogger Tips
Mh. Anne Makinda: Spika wa Bunge la TanzaniaHatimaye wabunge leo wameweza kumchagua spika ambaye ataongoza bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano.

Mheshimiwa  Anne Makinda ndiye spika Mpya wa Bunge baada ya kumshinda Mh. Mabere Nyaucho Marandu katika uchaguzi wa kumpata spika mpya wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Mama Makinda kapata kura 265 wakati Mh. Marando kapata kura 53.

Hivi sasa spika huyo mpya anasimamia zoezi la kuapa la wabunge wapya wa bunge hili la 10.

 Bunge la tisa lilimaliza muda wake juai 16, 2010. zoezi la kuapa wabunge wapya linatarajiwa kuchukua siku zaidi ya 2.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits