Tuesday, November 9, 2010

Best Blogger Tips
Wabunge Viti Maalumu

. CCM 65, CHADEMA 23 na CUF 8

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha kazi ya kuwateua wabunge wa awali wa Viti Maalumu na kuwasilisha orodha ya wateule hao katika vyama husika vya siasa.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata kutoka ndani ya NEC na miongoni mwa viongozi wa juu wa vyama vitatu vya siasa vyenye wabunge wa Viti Maalumu wamethibitisha kupokea majina ya wabunge hao.

Kwa mujibu wa habari hizo, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata wabunge 65 wa Viti Maalumu, kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichopata viti 23 na Chama cha Wananchi (CUF) kikapata viti vinane.

Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa, idadi hiyo ya viti maalum ambavyo jumla yake ni 96 itaongezeka kwa kila chama baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ulioahirishwa wa wabunge katika majimbo saba.
Chama cha NCCR Mageuzi kilichopata viti vinne vya wabunge, TLP na UDP kimoja, havikupata kiti hata kimoja cha wabunge wa viti maalumu kutokana na kukosa sifa ya kufikisha asilimia tano ya kura za wabunge wote kwa mujibu wa sheria.

Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara) na Conchesta Rwalumulaza (Kagera).

Wengine ni Suzan Kiwanga (Morogoro), Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam).
Majina mengine ya wateule hao ni Chiku Abwao (Iringa), Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).

Wabunge hao ambao wanatarajia kusafiri kwenda mjini Dodoma kuungana na wenzao, wanafanya idadi ya wabunge wote wa CHADEMA hadi sasa kufikia 45.

Kwa mujibu wa habari hizo idadi hiyo inakifanya chama hicho kiwe na sifa ya kuunda kambi ya upinzani bila kutegemea wabunge wa kutoka vyama vingine vya upinzani.

Kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho hata hivyo majina ya washindi hayakuweza kupatikana, kimepata idadi ndogo ya viti tofauti ilivyotarajiwa.
Endelea kusoma habari hii...............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits