Tuesday, November 16, 2010

Best Blogger Tips
Waziri Mkuu ni Mizengo Kayanza Peter Pinda



Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua mbunge wa Katavi mkoani Rukwa, Mizengo Kayanza Peter Pinda, kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika Anne Makinde alimtangaza Mh. Mizengo Pinda kuwa Waziri Mkuu Mteule jioni ya leo bungeni Dodoma. Baadaye kura za kumdhibitisha zikapigwa na matokeo ni kwamba: kura zilizopigwa: 328 kura za ndio: 277 (85.4%), kura za hapana: 49 (14.9%), kura zilizoharibika 2 (0.2%).

Waziri mkuu anatarajiwa kuapishwa kesho ikulu ndogo ya chamwino, ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kutangazwa kwa baraza jipya la mawaziri. hatua hii inakamilika baada ya rais kukaa na kushauriana na makamu wa rais na waziri mkuu.

Baraza hilo jipya linatarajiwa kutangazwa ijumaa.


No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits