Sunday, November 7, 2010

Best Blogger Tips
Mkakati waundwa kummaliza Sitta

Via Majira

KUNDI la watu wanaodaiwa kuwa ni mahasimu wa kisiasa linadaiwa kuanza mikakati mizito kuhakikisha linamwangusha Spika wa Bunge anayetea nafasi yake Bw. Samwel Sitta.

Vyanzo vyetu ndani ya CCM makao Makuu vilieleza Majira Jumapili kwamba kundi hilo tayari limeanza kutekeleza mkakati wake wa kwanza wa kutuma watu wake kuwania nafasi hiyo ili kupambana  na Bw. Sitta.

Mkakati wa pili wa kundi hilo wa kumwangusha Bw. Sitta ulitajwa kuwa ni kushawishi wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho (CC) itakayokutana kati ya Novemba 10 au 11 mjini Dodoma kukataa jina Mbunge huyo wa Urambo Mashariki.

"Tayari watu wao wawili wamechukua fomu kupambana na Mhe. Sitta, lengo ni kuhakikisha wanapata watu hata 10 kuchuana naye ili wakifika kwenye Kamati Kuu waseme kwamba hafai na ili wananchi wasipate nafasi ya kuhoji kama ameonewa wataachwa wengi.

"Wameanza kuwazungukia wajumbe wa Kamati Kuu na wapo wazee wachache wanawaunga mkono akiwemo kigogo mmoja wa chama,"kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

Hadi sasa waliokwishachukua famu ya kupambana na Bw. Sitta katika nafasi hiyo ni pamoja na aliyekuwa Naibu wake Bi. Anna Makinda, Bw. Andrew  Chenge, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Bw. Job Ndugai, Mbunge wa Afrika Mashariki Bi. Kate Kamba pamoja na Bi. Anna Abdallah. 
Endelea kusoma habari hii........................

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits