Friday, June 11, 2010

Best Blogger Tips
Afrika Kusini yatoka sare 1-1 na Mexico

Wenyeji Bafana Bafana wa Afrika Kusini watoka sare 1-1 na Mexico katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia.

Afrika Kusini wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia walianza mashindano hayo Ijumaa kwa kutoka sare 1-1 na Mexico katika mechi ya ufunguzi iliyokuwa na kandanda la kusisimua kabisa baina ya timu hizo mbili. Katika mechi ya pili ya kundi A Ijumaa Ufaransa na Uruguay zilitoka sare 0-0 katika mechi ambapo Uruguay walimaliza mchezo wakiwa wamebakiwa na wachezaji kumi tu baada ya mchezaji wao mmoja kupigwa kadi nyekundu.

Winga wa Afrika Kusini Siphiwe Tshabalala alifunga goli la kwanza katika fainali za mwaka huu katika dakika ya 55 katika uwanja wa Soccer City. Lakini mlinzi wa Mexico Rafael Marquez alipata bao la kusawazisha katika dakika ya 79 ya mchezo.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits