Friday, June 4, 2010

Best Blogger Tips
Joran Van der Sloot Akamatwa


Joran Van der Sloot, ambaye alikuwa mtuhumiwa mkuu wa kupotea kwa Natalee Holloway katika nchi ya Aruba mwaka 2005, amekamatwa nchini Chile kwa tuhuma ya mauaji yaliyotokea Lima, Peru.

Joran Van der Sloot, anatuhumiwa kumuua msichana mwenye umri wa miaka 21, Stephany Flores, ambaye mwili wake uliokuwa umejaa damu ulikutwa hotelini ndani ya chumba ambacho kilihusishwa na Van der Sloot.

Van der Sloot, amekanusha tuhuma hizo, ingawa amekili kwamba alikutana na Flores kwenye Casino ya Lima, msemaji wa polisi amethibitisha.

Bado ni mtuhumiwa mkuu wa kupotea kwa Natalee Hollway, mwanafunzi kutoka Mountain Brook, Alabama, aliyepotea nchini Aruba, akiwa katika mapumziko ya kusherehekea kumaliza shule.

Van der sloot, hakuwahi kushitakiwa kwa kupotea kwa Natalee Hollway, kwa sababu kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits