Saturday, June 19, 2010

Best Blogger Tips
Mwalimu afa akifuata mshahara

Via Majira

WATU wawili wamefariki akiwemo mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kivisini baada ya kuangukiwa na mti wakati wakiendesha baiskeli kwenda mjini kuchukua mshahara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mwanga, Bw. Willy Njau alitoa taarifa hiyo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo.

Mwalimu huyo ni Edmund Mtungo na mkulima Gerald Aloyce ambaye alifariki akipatiwa matibabu katika zahanati ya Kifaru wilayani hapa.

“Wakiwa kwenye baiskeli, bahati mbaya mti ulianguka ghafla na kumgonga mwalimu Mtungo na kufariki papo hapo huku mkulima akijeruhiwa vibaya kichwani na maeneo mengine mwilini, lakini
baadaye naye alikufa akipatiwa matibabu,” alisema.

Miili ya marehemu wote wawili imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya usangi ikisubiri mazishi yao ambayo yatafanyika Kilomeni na Kivisini.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits