Thursday, June 3, 2010

Best Blogger Tips
Mandela kuhudhuria Kombe la Dunia

Via BBC

Waziri wa michezo wa Afrika Kusini amesema, aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nelson Mandela atahudhuria ufunguzi wa sherehe za Kombe la Dunia.

Makhenkesi Stofile amesema Mandela mwenye sifa ya kupinga ubaguzi wa rangi aliomba tiketi kwa ajili ya siku ya ufunguzi na kufunga mashindano hayo.

Awali Mandela alisema alikuwa mdhaifu sana kuhudhuria shindano hilo linaloanza wiki ijayo.

Bw Mandela atakayefikisha umri wa miaka 92 mwezi ujao, alifanya kampeni ya kutaka Kombe la Dunia kufanyika Afrika Kusini.

Bw Stofile amesema, "Mandela ametaka kuhudhuria Kombe la Dunia."

Shirika lake la hisani, Mandela Foundation, halijathibitisha kuhudhuria kwake, wakieleza kuwa ni kutokana na sababu za kiusalama.

Takriban watu 350,000 wanatarajiwa kutembelea Afrika Kusini kwa ajili ya Kombe la Dunia, ambapo inafanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits