Sunday, June 13, 2010

Best Blogger Tips

JK kukutana na watoto kesho

Via ippmedia  

Rais Jakaya Kikwete kesho anatarajiwa kukutana na watoto jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine watamuuliza maswali zaidi ya 20 likiwemo kwa nini serikali haijasajili Baraza lao la Watoto lililoanzishwa miaka minane iliyopita.

 Katika mazungumzo hayo watoto pia watamhoji Rais Kikwete juu ya nini kinafanywa na serikali ili kupunguza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto, unyonyaji, kuongezeka kwa mimba za utotoni na mikakati ya kuwaondoa mitaani.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, mtoto Rehema Abbas atakayeongoza watoto kumhoji Rais, alisema katika mahojiano hayo watoto kumi watawawakilisha wenzao wanaokaribia nusu ya watanzania wote kwa sasa. 

 

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits