Tuesday, June 15, 2010

Best Blogger Tips
Ivory Coast yatoka sare na Ureno

Ivory Coast imetoka sare 0-0 na Ureno kwenye mechi ya kundi G la Kombe la dunia, katika uwanja wa Nelson Mandela Bay mjini Port Elizabeth.

Ivory Coast iliudhibiti mchezo lakini umaliziaji wa Gervinho na Salomon Kalou ukakosa kuzaa matunda.

Mshambuliaji wa Ivory Coast Didier Drogba aliingia katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Salomon Kalou baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kumruhusu kufunga kifaa mkononi ili kulinda jeraha lake.

Hata hivyo kuingia kwa Drogba hakukufanikisha safu ya ufungaji, akibanwa na walinzi wa Ureno.

Awali katika mechi shuti la Cristiano Ronaldo liligonga mwamba.

Mechi ya Ivory Coast itakayofuata itakuwa dhidi ya Brazil siku ya Jumapili, kabla ya kumalizia michuano ya makundi dhidi ya Korea Kaskazini tarehe 25.

Mlinzi wa Ivory Coast Kolo Toure aliondoka uwanjani akichechemea baada ya kupata jeraha, na bado haijawa wazi ikiwa ataweza kushiriki michuano itakayofuata.

Refarii Jorge Larrianda aliwaonyesha kadi ya njano Cristiano Ronaldo na Guy Demel kwa kujibizana wakiambiana maneno yasiyokubalika.

Kundi la G linaelezewa na wengi kuwa kundi la 'kifo' , kwani mbali na Ureno na Ivory Coast, linajumuisha mabingwa mara tano wa kombe la dunia Brazil na Korea Kaskazini.
Source: BBC

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits