Sunday, June 20, 2010

Best Blogger Tips
Raia wa Australia hawaonekani Afrika

Via BBC

  Wasiwasi unazidi kuongezeka juu ya usalama wa wakurugenzi wa migodi ambao ni raia wa Australia kutokana na ndege yao kutokujulikana ilipo.

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Cameroon kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Abiria tisa walikuwepo kwenye ndege hiyo, akiwemo mmoja wa matajiri wakubwa wa Australia Ken Talbot.

Kundi hilo lilitoka katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde siku ya Jumamosi kutembelea miradi ya madini ya chuma huko Yangadou, eneo lililo kijijini huko Kongo.

Jeshi la Cameroon linaongoza msako wa ardhini na angani kwenye msitu mkubwa sana.Ndege waliyokuwa wakisafiria lilikodishwa na kampuni ya migodi ya Australia, Sundance Resources.
Endelea kusoma habari hii............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits