Tuesday, June 1, 2010

Best Blogger Tips
Namibia yashtakiwa kwa kuhasi


Wanawake watatu Namibia wanaishtaki serikali kwa madai ya kuhasiwa bila idhini yao baada ya kupimwa na kuonekana na virusi vya ukimwi.

Wanawake hao wanasema madaktari na wauguzi walitakiwa kuwaelea uzuri kitu gani kilikuwa kikiendelea.

Shirika la utetezi linalowawakilisha, the Legal Assistance Centre LAC, limesema limekusanya ushahidi kutoka kesi 15 za madai ya kuhusika na kuhasiwa baada ya kuonekana na virusi vya HIV katika hospitali tangu mwaka 2008.

Maandamano ya kuwaunga mkono wanawake hao inaendelea huko Windhoek huku kesi ikianza.

Mwandishi wa BBC Frauke Jensen aliyopo kwenye mji mkuu huo, amesema kuna takriban waandamanaji 300.

Wengi wao ni wanawake, wakiwa na kauli mbiu yao " Mwili wangu, fuko langu la uzazi, haki yangu," na wakishika mabango yakisema: " Kwanini umenihasi?"

Pia wana mpango wa kufanya maandamano mengine siku ya Jumatano katika hospitali mbili ambapo inadaiwa shughuli hizo za kuhasi zilipofanyika.
Endelea kusoma habari hii...........

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits