Thursday, June 3, 2010

Best Blogger Tips
Lakers waifunga Celtics , 102-89, kwenye mchezo wa kwanza wa Fainali za NBA


Lakers wameanza vizuri mchezo wao wa kwanza kwa kuifunga Celtics, 102-89, katika mchezo uliofanyika Staples Center, Los Angeles.

Wakicheza kwa kujiamini, Lakers wameonyesha ni jinsi gani ambavyo hawataki kupoteza ubingwa wao waliouchukua mwaka jana.

 Alikuwa ni Kobe Bryant ambaye ndiye aliyewasumbua sana Celtics akitoka na points 30 na 7 rebounds, Paul Gasol (BigMan), alifanya kazi ya ziada akiwa na 14 rebounds, na points 23, huku Mchezaji aliyetoka Houston Rockets, Ron Artest akitoka na points 15 katika ushindi huo dhidi ya Boston Celtics.

Mchezo wa pili utafanyika tena Staples Center, Los Angeles, siku ya jumapili.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits