Tuesday, June 8, 2010

Best Blogger Tips
Mwalimu mwingine adaiwa kuoa mwanafunzi wake

SIKU chache baada ya mwalimu mmoja wa shule ya Sekondari ya Byuna wilayani Bariadi mkoani Shinyanga kukamatwa kwa kufunga ndoa na mwanafunzi wake, mwalimu mwingine wa Sekondari ya Nyakabindi wiyalani humo pia amebainika kuoa mwanafunzi wake baada ya kumtia mimba na kuishi naye kama mke.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa timu ya waandishi wa habari ambao waliambatana na maofisa wa Shirika la Utu Mwanamke katika utafiti wa mimba za utotoni wilayani Bariadi, Mwalimu huyo (Jina linahifadhiwa) ambaye ni makamu mkuu wa shule anadaiwa kuwa anaishi na mwanafunzi huyo tangu mwaka 2008 baada ya kupata ujauzito.

Mwalimu huyo anadaiwa kumpatia ujauzito mwanafunzi (Jina linahifadhiwa) ambaye inaelezwa kuwa alikuwa akisoma shule hiyo Nyakabindi, lakini kutokana na kuwa na mahusiano ya siri ya mapenzi na mwalimu wake alipata mimba na hivyo kuamua kumuoa kwa siri ambapo sasa anaishi naye.

Wakizungumza baadhi ya wanafunzi ambao walikuwa wakisoma na mwanafunzi huyo walieleza kuwa wakiwa kidato cha pili mwaka 2008 walikuwa wakisoma na mwanafunzi huyo, lakini aliacha shule katika mazingira ya kutatanisha ambapo baada ya muda walianza kumuona nyumbani kwa mwalimu na akiwa na mtoto.
Endelea kusoma habari hii...............

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits