Tuesday, April 26, 2011

Best Blogger Tips
Dhulma nchini Libya kufanyiwa uchunguzi

Via BBC

Kundi la maafisa kutoka Umoja wa Mataifa limetumwa mjini Tripoli kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Libya.

Jopo hilo liliteuliwa na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa punde tu utawala wa Libya ulipoanza kushambulia waandamanaji wanaompinga kanali Muammar Gaddafi.

Serikali ya Libya imesema itashirikiana na jopo hilo la wachunguzi ambalo pia litachunguza madai ya dhulma zilizotekelezwa na waasi na majeshi ya Nato.

Kuna taarifa kuwa tangu maandamano ya kumpinga Kanali Gaddafi yaanze watu wametoweka, wengine wameteswa na hata kuuawa.

Kamishna wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Navi Pillay alisema kuwa huenda uhalifu dhidi ya binadamu unafanyika nchini Libya tangu mzozo huo uanze.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu elfu moja wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Meli zimekuwa zikiwasafirisha watu waliojeruhiwa hadi mjini Benghazi kupata huduma za matibabu.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits