Monday, April 11, 2011

Best Blogger Tips
Majeshi ya Ufaransa 'yamkamata Gbagbo'

Via BBC

Mshirika wa Gbagbo alisema, wanajeshi wa Ufaransa wamemkamata kiongozi wa Ivory Coast Laurent Gbagbo kutoka kwenye makazi yake na kumkabidhi kwa upinzani.

Inaripotiwa kuwa waliingia baada ya vifaru vya Ufaransa kuingia katika makazi yake kwenye mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan, kufuatia mashambulio ya helikopta ya Ufaransa na Umoja wa Mataifa.

Bw Gbagbo alikataa kukabidhi madaraka kwa Alassane Ouattara, anayetambuliwa kimataifa kuwa mshindi wa urais nchini humo.

Majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kutunza amani yanayashutumu majeshi ya Bw Gbagbo kuhatarisha maisha ya raia.

Msemaji wa Rais Toussaint Alain aliliambia shirika la habari la Reuters kutoka Paris, "Gbagbo amekamatwa na majeshi maalum ya Ufaransa nyumbani kwake na amekabidhiwa kwa wapinzani."

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits