Friday, December 11, 2009

Best Blogger Tips
Tiger Woods


Habari ambazo zinachukua nafasi kubwa katika vyombo vya habari sasa hivi ni kwamba mcheza gofu namba moja Duniani, Tiger Woods, ameamua kupumzika kwa muda usiojulikana kucheza gofu.

“Baada ya kufikilia sana, nimeamua kupumzika kwa muda usiojulikana kucheza gofu. Nataka kuelekeza nguvu zangu katika kuwa mume na baba bora” Amesema Woods.

Habari hii imekuja wiki mbili baada ya kupata ajari ya gari ambayo ilikuwa na maelezo ya kuchanganya sana. Tuhuma za kujihusisha na wanawake wa aina mbalimbali nje ya ndoa zilianza kujitokeza, huku mwanamke mmoja akiwa na ushahidi wa kuachiwa message kwenye simu yake na Woods kabla ya ajari hiyo.

“Nafahamu kwa kiasi kikubwa sana kwamba kitendo cha kutokuwa mwaminifu katika ndoa, kimewaumiza watu wengi hasa mke wangu na watoto” Amesema Woods. “Naomba samahani kwa watu wote, siyo rahisi kurekebisha kosa nililofanya, lakini nataka kujitahidi kwa uwezo wangu wote”.

Woods na mke wake Elin, wana miaka mitano tangu wafunge ndoa, pamoja wana binti wa miaka miwili na mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi kumi.

2 comments:

Anonymous said...

Hbari nilizosikia mke wake anataka kuondoka hapo, kama ni kweli hali ni mbaya sana kwa Woods.

willymwamba said...

inatakiwa afanye kama kobe...alirudi akachukua championship ...watu wakasahau!..


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits