Sunday, March 21, 2010

Best Blogger Tips
Bilioni 300 zaibiwa kimafia Dar

WATU wasiofahamika wameghushi nyaraka za malipo na kuiba zaidi ya Sh300 bilioni katika benki tatu kubwa nchini na kusababisha mtikisiko mkubwa katika sekta ya fedha, uchunguzi umeonyesha.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, kwa njia ya mtandao wa kompyuta na kuhusisha wezi wa kimataifa ndani na nje ya nchi.

Tukio hilo ambalo ni kubwa kuwahi kutikisa sekta ya fedha nchini tangu uhuru mwaka 1961, limetokea katika kipindi cha takribani miaka miwili tangu serikali ianzishe kitengo maalumu cha Intelejensia cha kufuatilia Mzunguko wa Fedha chafu (FIU).

Licha ya kuwepo FIU, ambayo iliundwa pamoja na Sheria ya Kupambana na Fedha Chafu ya mwaka 2007, uchunguzi wa Mwananchi, umebaini kutokea wizi huo mkubwa katika benki hizo.

Uchunguzi huo umebaini kwamba, taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo ambazo ni mara tatu ya zile za EPA zilizoibwa katika Benki Kuu Tanzania (BoT), zilihamishwa kwa njia ya kompyuta kwa kughushi malipo kwenda kwa wahusika wa mtandao huo katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako Polisi wa Kimataifa wa nchini na wenzao wanahaha kuzichunguza.
Endelea kusoma habari hii......

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alithibitisha kuwepo taarifa za uhalifu huo, lakini akaweka bayana, hakuna ushahidi wa kiwango maalumu kilichoibwa hadi sasa.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits