Monday, March 15, 2010

Best Blogger Tips
Irene Uwoya aweka wazi alipokutana na mumewe

“ SANAA imekuwa na faida kubwa sana, faida ya kwanza ni kunipatia mume. Kupitia fani ya uigizaji ndipo mumewangu aliponiona na kunipenda” anasema muigizaji Irene Uwoya huku akitabasamu.

“ Nikweli kupitia uigizaji katika filamu ya Oprah, mumewangu akaniona na kunipenda na hatimaye sasa tumeoana,” anasisitiza.

Irene ambaye anatikisa katika fani ya uigizaji kutokana na mafanikio ya kuvaa uhusika, amefunga ndoa na mchezaji wa mpira wa miguu, Hamad Ndikumana ambaye ni raia wa Rwanda.

Ndikumana ambaye mbele ya mashabiki wa nchini mwake anajulikana kama Kataut, ni beki wa kimataifa wa Amavubi, ambaye kwa sasa anachezea soka ya kulipwa klabu ya Daraja la Kwanza ya A. E. Lemesos ya Cyprus.

Ndoa ya nyota hao ilifungwa mwaka jana kwenye Kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam. Irene ambaye ni mtoto wa kwanza wa familia ya Naima Mrisho na Pacras Uwoya, alizaliwa Desemba 18, 1988 mjini Dodoma, na kuanza elimu ya msingi katika Shule ya Mlimwa hadi darasa la tatu alipohamia Bunge ya Dar es Salaam alikomalizia elimu yake hiyo.
Endelea kusoma habari hii.....

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits