Monday, March 22, 2010

Best Blogger Tips
Sitta apuuza tuhuma dhidi yake, adai ni mchezo mchafu

BAADA ya kurushiwa tuhuma kadhaa, Spika wa Bunge la Muungano, Samuel Sitta amejitokeza na kudai kuwa amebaini kuna ni mchezo mchafu wa kutaka kumchafua katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.


Sitta, ambaye ameliongoza Bunge katika kipindi ambacho kashfa nyingi zimeibuliwa dhidi ya serikali na watendaji wake, amesema baada ya kubaini hilo sasa hatajibizana na kila mtu anayeibuka kumshambulia.

Spika Sitta ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho amekuwa akishambuliwa na watu mbalimbali huku sakata la utoaji wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura kwa kampuni ya Richmond Development LLC likitafsiriwa kuwa linatokana na tofauti baina yake na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Huku uchaguzi mkuu ukikaribia, katika tuhuma za karibuni, Sitta amejikuta akituhumiwa kufanya matumizi mabaya ya ofisi yake, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa samani za ofisi pamoja na kujipangishia nyumba kwa gharama kubwa.

Lakini Sitta alipuuza hoja hizo akisema kuwa zinatolewa kwa lengo la kumchafua, huku ofisi yake ikitoa ufafanuzi wa tuhuma zote katika majibu ya maswali iliyotumiwa na gazeti hili.

"Aaa nimebaini kuna ni mchezo mchafu tu dhidi yangu, mambo mengi yanayosemwa tayari yalikwishafafanuliwa na ofisi yangu," alisema Spika Sitta, ambaye ni mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki.
Endelea kusoma habari hii........

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits