Thursday, March 11, 2010

Best Blogger Tips
Mtoto azinduka kabla ya maziko

BAADHI ya madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam, wanadaiwa kutoa taarifa za uongo kwamba mtoto aliyezaliwa amekufa, lakini muda mfupi baadae alibainika kuwa yu hai. Tukio hilo lililoacha maswali mengi lilitotokea juzi saa moja usiku, ambapo uongozi wa hospitali hiyo ulithibitisha kutokea, huku ukitia shaka juu ya mazingira yake. Habari zilizopatikana hospitalini hapo zilidai mjamzito aliyejifungua mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo kichanga hicho cha kiume kikiwa kimeanza kutoka. Ilidaiwa baada ya mjamzito huyo kusaidiwa na kumaliza kujifungua, alielezwa mwanawe amekufa, hivyo walikabidhiwa kichanga hicho kwa ajili ya maziko. Kwa mujibu wa chanzo cha habari, baada ya kufika nyumbani wakijiandaa na mazishi ya mtoto huyo, baba yake alipewa taarifa za kifo na aliomba asizikwe hadi atakapofika. Ilidaiwa baada ya baba huyo kufika nyumbani, mtoto huyo aliyekuwa amefunikwa nguo alipofunuliwa alionyesha dalili za kuwa hai, huku akijinyoosha, jambo lililowafanya wamrudishe hospitalini hapo. Chanzo hicho kilidai baada ya kufikishwa hospitalini, kichanga hicho kiliwekwa kwenye kifaa maalumu kinachotumika zaidi kwa watoto njiti.
Kwa habari zaidi ingia hapa.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits