Monday, March 15, 2010

Best Blogger Tips
Mfalme Simba, Barasa aivua Yanga ubingwa apiga mbili


MSHAMBULIAJI Mike Barasa alifunga mabao mawili na kuisaidia Simba kutwaa ubingwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Mabao hayo mawili ya Barasa yalitosha kuivua ubingwa Yanga ambayo leo itacheza dhidi ya Moro United wakiwa na lengo la kutunza rekodi ya kutokufungwa raundi hii ya pili.

Simba iliyokuwa ikihitaji pointi mbili kujitangazia ufalme, iliuanza mchezo huo dhidi ya ndugu zao Azam kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika kila kipindi.

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Mike Barasa aliyejiunga na Simba wakati wa dirisha dogo alipachika bao lake la kwanza dakika 7, na lile la pili dakika 62, ya mchezo.

Mchezaji Hillay Echessa akiwa pembani ya uwanja alipitisha krosi nzuri iliyounganishwa kwa kichwa na Barasa na kumwacha kipa wa Azam Vladmir Niyonzima asijue la kufanya.

Kabla ya kupokea pasi nzuri ya mbali kutoka kwa Uhuru Selemani aliyoiunganisha kwa shuti kali lilokwenda moja kwa moja wavuni dakika 62.
Endelea kusoma habari hii......

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits