Friday, March 26, 2010

Best Blogger Tips
Muungano wa upinzani washinda kura Iraq

Via BBC

Muungano wa vyama vinavyomuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq Iyad Allawi vinaongoza kwa idadi ya viti katika uchaguzi wa ubunge.

Muungano huo umepata viti 91 dhidi ya 89 vya chama kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa sasa Nouri Maliki.

Matokeo hayo yamewashangaza wengi na kumwacha Bwana Maliki akinung’unika akisema sharti kura zihesabiwe upya na kwamba ataendelea  na mipango yake ya kuunda serikali mpya.

Tayari mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ameyataja matokeo hayo kuwa ya kuaminika na akawahimiza raia wa Iraq kuyakubali.

Itambidi Bwana Allawi kuunda serikali ya muungano huku kukiwa na wasiwasi kwamba huenda matokeo hayo yakazusha machafuko.

Muda mfupi kabla ya matokeo hayo kutangazwa, kulitokea milipuko miwili ya mabomu kwenye mji wa Khalis na kuwaua watu wapatao 40.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits