Wednesday, February 17, 2010

Best Blogger Tips
17 waliokatwa mapanga Tanzania wazikwa

Watu hao wa ukoo mmoja waliouawa usiku wa kuamkia Jumanne mjini Musoma,kaskazini mwa Tanzania wamezikwa Jumatano jioni.

Maelfu ya wananchi walihudhuria maziko hayo,huku serikali ya Tanzania ikiahidi kuwasaka watuhumiwa wa mauaji hayo.

Nyasinde Kawawa, msichana mwenye umri wa miaka 21 alikuwa mwenye huzuni kubwa huku majeneza 17 yakiwekwa mbele ya nyumba.

Babake,mamake,ndugu zake watano na binamu yake wote waliuawa kwenye tukio hilo.

Nyasinde alinusurika kifo kwa kuwa ameolewa na anaishi mbali na nyumbani kwao.

Source: BBC

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits