Thursday, February 4, 2010

Best Blogger Tips
Daktari wa Michael Jackson kujisalimisha.Wakili wa aliyekuwa Daktari wa Michael Jackson, anaongea na mteja wake ili aweze kujisalimisha kwenye Mamlaka ya sheria katika Jiji la Los Angeles.

Katika ripoti yake aliyoitoa siku ya alhamisi, Wakili Ed Chetnoff, amesema anafanya mazungumzo na ofisi ya Mwanasheria wa Los Angeles kwa ajili ya kujisalimisha kwa Conrad Murray.

Maafisa wa sheria waliiambia Associate Press kwamba, upande wa mashitaka una mpango wa kumshitaki Murray kwa kosa la Uuaji wa bila kukusudia kwa kumpa Jackson dawa zenye nguvu kubwa za anesthetic, zilizopelekea kifo chake mwezi wa sita mwaka huu.

Murray hajashitakiwa bado, anategemewa kupelekwa mahakamani siku ya ijumaa. Maafisa hao walikuwa wanazungumza kwa sharti la kutotaja majina, kwa ajili ya umuhimu wa kesi hiyo.

Murray amesisitiza kwamba hajampa kitu chochote kibaya Michael Jackson ambacho kilisababisha kifo chake.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits