Tuesday, February 16, 2010

Best Blogger Tips
Kenya; ODM kususia mikutano


Tofauti za kisiasa nchini Kenya inaelekea zinaendelea kuzidi, na chama cha waziri mkuu Raila Odinga sasa kikielezea kitasusia vikao vya baraza la mawaziri hadi suluhu itakapopatikana.

Ubishi ulianza mwishoni mwa wiki, waka Rais Mwai Kibaki alibatilisha uamuzi wa waziri mkuu Raila Odinga kuwasimamisha kazi mawaziri wawili, kuhusiana na madai ya kashfa za ufisadi.

Mwandishi wa BBC wa Afrika Mashariki ameelezea kwamba hali hiyo ni ya kutia wasiwasi, kwani ni dalili ya kuelekea kuporomoka kwa serikali ya mseto.

Serikali hiyo ya pamoja ilianzishwa miaka miwili iliyopita, kufuatia vifo vya watu 1500 katika ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits