Monday, February 1, 2010

Best Blogger Tips
Grizzlies waifunga Lakers

 Grizzlies, team ambayo Hasheem Thabeet anachezea, leo wameweza kuifunga team ngumu ya Lakers kwa 95-93. Grizzlies, team ambayo ilikuwa haipewi kabisa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya NBA, imekuwa tishio kubwa sana hasa inapocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Mpaka sasa hivi team hiyo imeshinda mechi 25 kati ya 46 ilizocheza. Licha ya Kobe Bryant kupata points 44 katika mchezo huo, haikuweza kuwazuia vijana hao wa Memphis kuweza kuibuka na ushindi na kuwaacha vijana toka LA kutoamini macho yao.

Kesho wana game ngumu dhidi ya Cleveland Cavaliers. Cavaliers ndio wanaoongoza kwa upande wa East kwa sasa hivi, wakiwa na mkali wao Lebron James na mkongwe Shaq O'neal.

1 comment:

Anonymous said...

Mbona Hasheem simuoni akicheza mara kwa mara, naona anapewa muda mchache sana wa kucheza!!


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits