Tuesday, February 16, 2010

Best Blogger Tips
Sanamu ya Obama yahamishwaJakarta, Indonesia;
Sanamu ya Rais Barack Obama iliyokuwa kwenye bustani katika mji mkuu wa Indonesia, iliondolewa na kupelekwa kwenye shule ambayo Rais huyo alisoma wakati akiwa mtoto.

Sanamu hiyo iliyotengenezwa kwa shaba, iliundwa kulingana na rais huyo akiwa na miaka 10. Sanamu hiyo ilikuwa imelengwa na wakosoaji tangu ilipowekwa kwenye bustani hiyo mwaka jana. Wakosoaji hao walisema kwamba shujaa wa nchi hiyo ndiyo angepatiwa heshima hiyo kwani rais Obama huenda bado akafuatilia sera ambazo zitaumiza matakwa ya Indonesia.

Rais Obama ambaye mama yake ni mmarekani aliolewa na mwanamme raia wa Indonesia baada ya kutalikiana na baba yake Obama raia kutoka Kenya. Alisoma katika mji huo kanzia mwaka 1967 hadi 1971 na anathaminiwa na watu wengi wa Indonesia.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits