Thursday, February 18, 2010

Best Blogger Tips

Lundenga: Iacheni mahakama ifanye kazi zake

MRATIBU wa mashindano ya urembo, Hashim Lundenga amewataka Watanzania kuiachia mahakama ifanye kazi yake kwa uhuru na ione kama kweli mrembo wake ana hatia ama la.

Akizungumza na Mwananchi jana, Lundenga alisema kumekuwa na hoja kuwa Kamati ya Miss Tanzania imvue taji mrembo, kitu alichosema hakiwezekani.

Hatua ya Lundenga imekuja ikiwa ni siku moja baada ya mrembo wake, Miriam Gerald kuachiwa huru kwa kile kilichoelezwa kufanya shambulio la mwili na kuharibu mali na mtu mmoja anayeaminika kuwa ni rafiki yake.

Miriam aliyetwaa taji Oktoba 2, mwaka jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumshambulia Shaaban Moshi kwa vitu vyenye ncha kali wakati shitaka la pili, ni kufanya uharibifu wa mali yenye thamani ya shilingi 720,000.No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits