Wednesday, February 17, 2010

Best Blogger Tips
Rais Mwai Kibaki akwepa mjadala

Rais Mwai Kibaki, jana alikwepa mjadala mkali unaoendelea kuhusu mzozo wa mamlaka kati yake na Waziri Mkuu. Badala yake, Rais alionekana kuchukulia hali kuwa shwali na badala yake kuzungumzia hali kuhusu kuimarisha uchumi wa nchi.

Alikuwa akizungumza katika kiwanda cha pombe cha EastAfrican Breweries, jijini Nairobi, wakati wa uzinduzi wa mtambo mpya wa kutayarishia bia. Jana ilikuwa shughuli yake ya kwanza ya hadhara tangu mambo yatumbukie nyongo kati yake na Bwana Odinga kuhusu kashfa za mahindi na elimu bila malipo, jumamosi iliyopita.

Rais Kibaki, alikataa katakata kugusia suala hilo wakati ambapo mashirika ya kijamii yalikuwa yakiandamana jijini kumshinikiza awafute kazi Bwana Sam Ongeri (Elimu) na Bwana Wiliam Ruto (Kilimo), ambao walisimamishwa na Bwana Odinga, lakini Rais akabatilisha uamuzi huo.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits