Tuesday, July 19, 2011

Baba adaiwa kumbaka mtoto wake Muheza

Best Blogger Tips
Via Mwananchi

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mkazi  wa Muheza, mkoani Tanga, (Jina limehifadhiwa), anadaiwa kumbaka mwanaye wa kumzaa mwenye umri wa miaka minne.Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa kufanyika miezi kadhaa iliyopita na kuripotiwa katika vyombo vya dola.Pamoja na kuripoti taarifa hiyo polisi  ilielezwa kwamba vyombo vya dola vimekuwa vikisuasua kufuatilia na kuchunguza ukweli juu ya tuhuma hizo.

Shemeji wa mlalamikiwa aliyejitambulisha kwa jina la Mbaruku Mwaita alisema taarifa za udhalilishaji watoto ziliripotiwa katika kituo cha polisi Chumbageni wilayani Muheza  siku nyingi, lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.Alisema  tatizo hilo lina  jalada namba MUH/IR/205/2011,  lakini tangu ilipofunguliwa hakuna dalili za kuendelea kwa kesi.

Mwaita, alisema  shemeji yake amekuwa na tuhuma za kufanya vitendo hivyo viovu mara kadhaa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, alipoulizwa jana kwa njia ya simu alikiri kupokea  jalada hilo  Julai 16 , mwaka huu.Massawe alisema  faili hilo litapelekwa kwa  Mwanasheria wa Serikali ili kuangaliwa na kuanza kwa kesi kama linajitosheleza.

Aliwataka wahusika kuwa na  subira  kutokana na ukweli kwamba polisi wanaendelea kushguhulikia na kwamba kesi itasikilizwa  kabla ya mwaka huu kuisha.Lakini, shemeji huyo wa mtuhumiwa akifafanua zaidi, alisema  mtuhumiwa mara ya kwanza alishafanya kitendo kama hicho kwa mdogo wake wa kike aliyekuwa anaishi naye awali jambo ambalo lilisababisha dada yake aombe talaka na shemeji huyo kuoa mke mwingine.

Mbaruku alisema  baada ya wawili hao kupeana talaka, mwanaume aling’ang’ania kukaa na mtoto wake akitaka akalelewe na mama wa kambo jambo ambalo lilizua mtafaruku, lakini alifanikiwa kuondoka na mtoto huyo.

 ‘’Baada ya mwezi mmoja kupita mtuhumiwa alimpiga simu mama ambaye ni bibi yake aende akamchukue mtoto stendi ya basi ,lakini mtoto yule alionyesha kudhoofu kwa kiasi kikubwa kiafya akawa akijisaidia haja ndogo anatoa damu jambo lilisababisha wampeleke hospitali."

Katika ripoti iliyotolewa na hospitali teule ya Muheza, inaoonyesha sehemu za siri za zimetanuka na kuathirika vibaya  kuliko umri wake na ikithibitishwa ni kweli ameingiliwa kimaumbile zaidi ya maramoja.

‘’Sikufichi hii kesi hata inavyoendeshwa kama familia hatujaafiki na tulishaandika barua ya malalamiko yaliyojibiwa kuna upungufu katika ushahidi uliotolewa , mshtakiwa alipokamatwa kwa mara ya kwanza alikaa polisi kwa  muda wa siku sita tu siku tuliyoenda tukaambiwa amepelekwa mahakama ya Tanga chumbageni lakini tulipofika tuliambiwa huyo mtuhumiwa hakufikishwa mahakamani turudi Muheza” alifafanua  Mbaruku.

Alifafanua kwamba,  huenda kesi hii haitendewi haki na wamekuwa wakizungushwa kila wanapofatilia mahakamani wanaambiwa kesi imeenda jambo ambalo si la kweli na kuongeza, wakati mwingine huambiwa ipo mahakamani hivyo si swala lao tena kwani kesi hiyo iko chini ya wakili wa serikali.

Mbaruku alisema kinachomsikitisha zaidi muhalifu anayekabiliwa kesi ya kubaka ametoka polisi kwa dhamana na akiendelea na shughuli zake kama kawaida.Tukio kama hili liliripotiwa mwishoni mwa  wiki iliyopita kutokea maeneo ya Kimara Suka ,ambapo  Hamisi Elia Minja  anadaiwa  kumuingilia kinyume na maumbile binti yake wa kuzaa mwenye umri wa miaka 10  huku akimtishia kumchoma na kisu wakati akimfanya kitendo hicho cha kinyama.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits