Saturday, July 23, 2011

Pumzika Kwa Amani Danny Mwakiteleko

Best Blogger Tips

Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Habari Corporation inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, The African na Rai, Danny Mwakiteleko amefariki dunia.

Mwakiteleko amefariki dunia saa moja asubuhi ya leo (Jumamosi Julai 23) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kufuatia ajali mbaya ya gari aliyoipata Julai 19, mwaka huu saa 5 usiku wa maeneo ya Tabata ya TIOT, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoka kazini kurudi nyumbani kwake, Tabata ya Baracuda.

Marehemu, akiwa kwenye gari lake aina ya Nadia, aliingia nyuma ya lori lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara.

Baada ya ajali hiyo, marehemu alipelekwa  Hospitali ya Wilaya ya Ilala, Amana ambako madaktari waliamua kumkimbiza Muhimbili kwa sababu hali yake ilikuwa mbaya.

Jana Ijumaa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete alimtembelea marehemu wodini Muhimbili alikolazwa kwa lengo la kumjulia hali.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Tabata Baracuda ambako pia mipango ya mazishi inafanywa.

Marehemu ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya, ameacha mke na watoto wawii, mmoja anasoma kidato cha pili, mwingine darasa la tano.

No comments:


Copyright 2011 Mambo ya Leo Blog. All Rights Reserved.
 

yasmin lawsuits